Kuhusu

Kuhusu

Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali ya Vijana (DEK Youth) ni nini?

Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali ya Vijana (Digital Enquirer Kit Youth) ni kozi ya mafunzo binafsi iwafundishayo watoto na vijana namna ya kutambua taarifa potofu, namna ya kutafuta, kukusanya, na kuchambua taarifa za kuaminika mtandaoni, na namna ya kuzishirikisha katika njia iliyo salama. Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali ya Vijana (DEK Youth) ni toleo lililojizatiti vilivyo na lililo rafiki kwa watoto kutoka kwenye toleo lake mama, Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer Kit), linaloweza kupatikana kupitia atingi.

 

‘Atingi’ ni nini?

Atingi ni jukwaa la mafunzo ya kidigitali lililotengenezwa na shirika la ‘Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH’ kwa niaba ya Wizara ya Maendeleo na Ushirikiano wa Kiuchumi. Kwa kutoa kozi za mafunzo mtandaoni bure zihusuzo stadi za kidigitali, uongozi na demokrasia, pamoja na mada nyinginezo kadhaa, atingi imekusudia kuwapatia wanafunzi wake maarifa na ujuzi wanaouhitaji kuboresha hali zao za maisha na kuongeza thamani kwa jamii zao.

 

Wasiliana nasi

Endapo kama utapenda kutupatia maoni yako